Kigango cha Mt. Fransisko wa Asizi

Taarifa fupi

Historia fupi

Parokia ya Mt. Fransisko Ksavieri ilizinduliwa rasmi tarehe 19 Desemba, 2015 na Mhashamu Baba Askafu Mkuu Beatus Kinyaiya OFM Cap. wa jimbo Kuu la Dodoma.
Paroko wa kwanza alikua Padre Magnus John Tegete C.PP.S na Paroko msaidizi ni Padre Gasper Baraka C.PP.S.
Parokia ilianzishwa ikikadiriwa kwuwa na waamini wanaoshiriki kikamilifu zaidi ya 4000.

Muundo wa Kigango

Bado maelezo

Jumuiya

Kigango ina jumuiya (6). Jumuiya hivyo ni:
Mt. Anna (block 3)
Mt. Fransisko wa Asare (block 6)
Mt. Yoseph Mfanyakazi (block 2)
Mt. Yohane Paulo II (block 4)
Mt. Yohane Bosco (block 1)
Mt. Anthony wa Padua (block 5)

Vyama vya Kitume

Kigango kina vyama vya kitume (5). Vyama hivyo ni:
Moyo Mtakatifu wa Yesu
Mt. Aloyce Gonzaga
Mt. Marko Mwinjili
Karsimatiki katoliki
Mt. Karoli Lwanga

Dira ya kigango

Dira ya kigango ni: KUJIBU KILIO CHA DAMU

Mpango wa kichungaji wa parokia yetu unamwelekeo wa kujibu kilio ha Damu kwa njia zifuatazo:
Maadhimisho ya Misa Takatifu, Sala na Kuhubiri neno la Mungu tukkiitikia mwito wa Bwana wetu Yesu Kristo. (Mk 16:15-16)

Matendo ya huruma. Tunashirikiana kuwa saidia wahitaji mbalimbali kimwili na kiroho kama vile watoto yatima, wagonjwa, wafungwa, walemavu, wanonyimwa haki zao, wasio na uwezo wa kiuchumi, wenyeshida za masomo au kifamilia, waliotengwa, waliofiwa na ndugu zao na wasiomwamini Kristo.

Semina mbalimbali, mafundisho ya dini na Sakramenti mbalimbali ili kuwezesha waamini kuwa wajumbe wa amani, upendo, ukarimu, umoja, huruma na upatanisho.